Mchezaji wa Brazil Marta amekuwa
mchezaji aliyeongoza kufunga magoli mengi katika michuano ya Kombe la
Dunia kwa Wanawake baada ya kupachika bao lake la 15 katika ushindi
wa mabao 2-0 dhidi ya Korea Kusini.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 29, ameingia katika rekodi hiyo baada ya kufunga goli lake kwa
njia ya penati, katika kipindi cha pili na kumpiku mshambuliaji wa
zamani wa Ujerumani Birgit Prinz.
Mchezaji mkongwe wa Brazil Formiga
alipachika bao la kwanza na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye
umri mkubwa kucheka na nyavu katika michuano hiyo akiwa na umri wa
miaka 37.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni