.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 10 Juni 2015

AFISA WA POLISI ALIYETUMIA NGUVU KULIKO DHIDI YA MSICHANA NCHINI MAREKANI AJIUZULU

Afisa wa polisi nchini Marekani ambaye alipigwa picha ya video akimpiga mweleka msichana mweusi na kumuangusha aridhini na kisha kumuelekezea bastola Jijini Texas amejiuzulu kazi.

Taarifa zinaeleza afisa huyo Eric Casebolt, amewasilisha barua ya kuacha kazi bila ya kushinikizwa na mtu hapo jana.

Katika video hiyo iliyorekodiwa Ijumaa huko McKinney polisi Casebolt, ambaye ni mzungu alionekana akimkandamiza chini kwa kutumia magoti binti mweusi wa miaka 15 aitwae Dajerria Becton. 

Polisi wamesema afisa huyo alikuwa ameenda kutuliza ghasia katika sherehe iliyokuwa ikifanywa kwenye bwawa la kuogelea katika eneo hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni