Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM
Taifa, wilaya Arumeru na Diwani wa Kata ya Mlangarini, wilayani
humo, Mathias Manga, amenusurika kufa, usiku wa kumakia leo, baada ya
kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kumuumiza maeneo ya mbavu za
kulia.
Akizungumza leo kwa njia ya simu,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea Juni 23 mwaka huu, majira
ya saa 4:45 eneo la Ngarenaro na majeruhi pia ni mfanyabiashara
mkubwa wa madini ya Tanzanite.
Amesema Manga alikuwa akitoka katika
shughuli zake za kawaida na alipokuwa anarejea nyumbani kwake eneo la
Ngarenaro, kwenye nyumba za Shirika la Nyumna la Taifa, ghafla aliona
gari likimfuata kwa nyuma na alipokuwa akitembea kwa kasi nalo
liliongeza mwendo.
Sabas amesema Manga akahisi hao watu
wanamfuata, hivyo akazidi kuongeza mwendo hadi alipofika getini kwake
nalo lilipaki kwa nyuma yake na akashuka mtu mmoja, akiwa ameshika
kisu na mara mwingine akiwa ameshika bunduki na ndipo alipolazimika
naye kutoa silaha yake yake.
Amesema Manga alipotoa silaha yake
ili kujiami, alishtukia amepigwa risasi na kwa bahati nzuri
haikumpata vizuri, ilimpitia maeneo ya nyama kwenye mbavu upande wa
kulia na watu hao waliondoka na walikuwa watano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni