Wataalam wa afya wamesema kuwa
kuendelea kwa mlipuko wa Ebola nchini Guinea kunarudisha nyuma
mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini humo.
Wataalam hao wanakadiria matukio
wagonjwa elfu 74 wa malaria ambao hawakutibiwa mwaka 2014, kutokana
na kufungwa kwa zahanati ama wagonjwa kuogopa kupatiwa tiba.
Wametahadharisha kuwa vifo vya
malaria tangu kutokea mlipuko wa Ebola, vitazidi mno idadi ya vifo
vya ugonjwa wa Ebola ambavyo ni watu 2,444.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni