Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi
nchini Kenya, Jenerali Samson Mwathethe, ameapa kuwafutilia mbali
magaidi wote katika mipaka ya Kenya.
Jenerali Mwathethe ametoa ahadi hiyo
jana mbele ya rais Uhuru Kenyatta, ambaye alienda kuwatembelea
hospitali wanajeshi wanane, waliojeruhiwa katika tukio la uvamizi la
Al-Shabaab kwenye kambi ya jeshi huko Lamu, siku ya jumapili.
Jenerali Mwathethe amemuambia Rais
Kenyatta mashujaa wake licha ya kujeruhiwa wanania ya kurejea katika
kambi hiyo tayari kwa vita hadi dakika ya mwisho ili kuhakikisha
wananchi wa Kenya wapo salama.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni