Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wadau wa michezo, wakati wa uzinduzi wa Kinondoni CUP uliofanyika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam jana ambapo pia aligawa vifaa vya michezo kwa timu 138 vikiwa ni seti mbili za jezi na mipira miwili kwa kila timu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wadau wa michezo katika uzinduzi huo.
DC Makonda akisisitiza jambo katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk.Aziz Msuya, Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Haroob, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwananyamala, Dk.Sophinias Ngonyani, Mdau wa Michezo, Alfan Kingama na Mwenyekiti waChama cha Jogging Wilaya ya Kinondoni, Abdul Mollel.
Mdau wa Michezo, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda ambaye alitoa mchango wa mipira 50, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwakilishi wa Kampuni ya TSN, Hamis Tembo akizungumza katika hafla hiyo. TSN ilitoa vifaa vyenye thamani ya sh.milioni 50 kuunga mkono jitihada za DC Makonda za kuanzisha mashindano hayo.
Vijana wa wilaya hiyo walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya wakiwa kwenye uzinduzi huo. Vijana hao hivi sasa afya zao zimeanza kuimarika baada ya kuanza kliniki maalumu iliyopo ndani ya Hospitali ya Mwananyamala.
Mdau William Malecela 'Limtuz' akizungumza katika uzinduzi huo. Limtuz ametoa mchango mkubwa wa kuujulisha umma kuhusu uzinduzi huo kupitia mitandao ya kijamii 'Asante Limtus kazi kazi nzuri"
Mdau wa mpira wa kikapu akikabidhiwa jezi na mpira na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Nahodha wa timu ya mpira wa kikapu ya Mbezi Beach, Shatiu Songoro (kushoto), akikabidhiwa vifaa vya michezo na DC Makonda.
Hapa ni sebene kwa kwenda mbele kutoka kwa wana jogging mbalimbali wakati wa uzinduzi huo.
Vifaa vya michezo vilivyotolewa na DC Makonda kwa vilabu mbalimbali katika wilaya hiyo.
Sehemu ya umati wa vijana na wadau wa michezo waliohudhuria uzinduzi huo. "Hongera Makonda kwa kazi nzuri"
Wana jogging wa wilaya hiyo wakishangilia hutuba ya DC wao Makonda. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni