.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Juni 2015

BERNARD MEMBE AHUDHURIA MSIBA WA MTOTO WA JENERALI MSUGURI NA KUHANI MSIBA WA JOHN NYERERE BUTIHAMA MKOANI MARA

SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri (wa tatu kulia), Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
SONY DSC 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akijadiliana jambo na Mama Maria Nyerere baada ya shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri, katika ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua. Kulia ni Mbunge wa Mchinga (CCM), Saidi Mtanda.
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati alipokwenda nyumbani hapo kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015.
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. John Guido Nyerere aliyefariki Mei 9 mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015.
SONY DSC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akitoka nje ya kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kuweka shada la maua wakati alipokwenda nyumbani hapo, kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. 

                                                                                           Picha zote na John Badi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni