Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa
ni wapiganaji wa kundi lenye kufuata itikadi kali za Kiislam la
al-Shabaab, jana usiku wamemuua Chifu mmoja nchini Kenya katika mpaka
wa kaskazini mashariki mwa mji wa Wajir.
Chifu huyo Mohammed Barre wa eneo la
Erib huko Wajir, alipigwa risasi na kufa na watu waliokuwa na silaha
waliokuwa wakimfuatilia wakati akitoka msikitini, ambako alienda
kuswali swala ya mwisho ya usiku.
Kamanda wa polisi wa kaunti ya
Wajiri Samuel Mukindia amethibitisha kuuwawa kwa chifu huyo
aliyemuelezea kuwa alikuwa mtumishi wa serikali muadilifu, ambapo
amesema alipigwa risasi umbali wa mita 500 kutoka msikitini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni