Mjumbe wa Mamlaka ya Taifa ya kupiga
Vita Matumizi ya Pombe na Dawa za Kulevya Kenya (Nacada) Charles
Njagua maarufu kama Jaguar amedai kuwepo kwa uozo mkubwa wa rushwa
katika mamlaka hiyo.
Jaguar ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe
wa Nacada karibu mwezi mmoja sasa, amesema amekuwa akikabiliwa na
upinzani mkubwa kwa kuhoji upotevu na matumizi yasiyo sahihi ya fedha
katika chombo hicho.
Akiongea katika mkutano kwenye ofisi
Jaguar ambaye pia ni msanii wa muziki Kenya amedai kuwa wajumbe wa
bodi ya Nacada na Kamati ya Fedha ni sehemu ya wahusika wa ubadhirifu
wa fedha wa chombo hicho cha kupiga vita pombe na dawa za kulevya.
Jaguar amewatuhumu baadhi ya wajumbe
wa bodi hiyo kwa kuchota kiasi cha shilingi milioni 500 za Kenya bila
ya kufanyiwa majadiliano na kuridhiwa na wajumbe wote wa bodi hiyo ya
Nacada.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni