Waziri wa Utamaduni wa Bolovia
amesema kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ameomba
kupatiwa fursa ya kutafuna majani ya coca, wakati wa ziara yake
itakayofanyika nchini Bolovia.
Coca ambayo ni moja ya viungo
vinavyotumika kwa ajili ya kutengenezea cocaine, yamekuwa yakitumika
kwa maelfu ya miaka kukabiliana na maradhi yanayowakumba watu
wanaokaa kwenye maeneo ya juu yenye miinuko na kuboresha saikolojia
ya mtu.
Rais Machicao amesema serikali ya
Bolovia ilimuahidi Papa kumpatia chai ya majani ya coca, hata hivyo
Papa ameomba kupatiwa fursa ya kutafuna majani ya mmea huo kama
wanavyofanya wenyeji wa nchi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni