Mwanamke raia wa Tanzania aitwae
Chambo Fatma Basil, amekamatwa katika uwanja wa ndege wenye harakati
nyingi wa Mumbai akiwa na kilo 74 za dawa za kulevya aina ya
methaqualone.
Maafisa wa Uhamiaji na wa Usalama
walimkamata mwanamke huyo, jumatano akiwa na paspoti ya Tanzania
akijianda kuja Dar es Salaam kupitia Doha, baada ya kupatiwa taarifa
za kishushushu.
Baada ya kufanyiwa upekuzi
ilibainika kwenye mabegi yake matatu kulikuwa na pakiti zenye unga
mweupe na uchunguzi zaidi ulibaini unga huo ni dawa za kulevya aina
ya methaqualone ama Mandrax, ambayo ni kilevi cha bei rahisi kuliko
cocaine.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni