Polisi wamesema watu wapatao 27
wamekufa baada ya kunywa pombe yenye sumu nchini India, magharibi mwa
Jiji la Mumbai (Bombay).
Wamesema kuwa wakazi wa makazi dunia
ya Malad, waliugua baada ya kunywa pombe hiyo siku ya jumatano
asubuhi.
Watu wengine 30 wanapatiwa matibabu
kwenye hospitali, huku kukiwa na hofu ya uwezekano wa vifo
kuongezeka.
Matukio ya pombe zenye sumu
hujitokeza mara kwa mara nchini India, ambapo watu hunywa pombe za
bei ya rahisi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni