Nchi ya Pakistani imeagiza shirika
la kusaidia watoto la Save the Children kuondoka nchini, ambapo
maafisa wa nchi hiyo wanalituhumu shirika hilo kwa kupingana na
serikali ya Pakistani.
Polisi wamezingira ofisi za shirika
hilo Jijini Islamabad na maafisa wa kigeni 15 wa Save the Children
wamepewa siku 15 kuondoka nchini humo.
Hata hivyo Shirika la Save the
Children limesema kuwa linapinga vikali uamuzi huo wa serikali ya
Pakistani.
Awali Pakistan ilihusisha shirika
hilo na programu feki ya chanjo iliyotumika na CIA katika kumnasa Osama Bin Laden.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni