Polisi nchini Marekani wameanza
msako wa kuwatafuta wafungwa Richard Matt, 48, na David Sweat, 34,
ambao wametoroka katika gereza lenye ulinzi mkali la Clinton lililopo
Dannemora, jana alfajiri.
Polisi wamesema wafungwa hao
walitumia mashine zenye uwezo mkubwa kukata chuma cha ukuta wa gereza
na kutoboa bomba kubwa na kisha kulitumia kutoka nje.
Msako huo unahusisha maafisa 200 wa
polisi ili kuhakikisha wanafanikiwa kuwatia nguvuni wafungwa hao
hatari.
Bomba walilokata wafungwa hao na kutumia kutorokea.
Waliacha Ujumbe huu katika bomba hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni