Rais Barack Obama wa Marekani
amesema viongozi wa G7 watazungumzia msimamo wao juu ya uvamizi wa
Urusi nchini Ukraine, wakati akiwasili kwenye
mkutano huo nchini Ujerumani.
Katika mkutano huo wa mataifa hayo
ya magharibi yenye nguvu za kiuchumi duniani pia utagusia masuala ya
biashara, ghasia za misimamo mikali ya kidini pamoja na mabadiliko ya
hali ya hewa.
Taifa la Urusi limeondolewa katika
kundi hilo ambalo awali lilikuwa likijulikana kama G8, tangu
kujitenga kwa jimbo la Crimea mwaka jana na kuunga mkono waasi wa
mashariki mwa Ukraine.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni