Mahakama ya Juu ya Saudi Arabia
imekazia hukumu ya kupigwa bakora 1,000 na kifungo cha miaka 10, jela
kwa bloga, Raif Badawi, licha ya mataifa ya kigeni kuipigia kelele
adhabu hiyo.
Akiongea nchini Canada, mke wa bloga
huyo Ensaf Haidar, ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa uamuzi
huo wa mahakama ya juu ni wa mwisho na hauwezi tena kubalishwa.
Mwezi Machi, mwaka huu utawala wa
kifalme wa Saudi Arabia ulionyesha kushangazwa na hatua ya mataifa ya
kigeni kuikosoa adhabu hiyo.
Aidha, Wizara ya Mambo ya Nje ya
nchi hiyo ilitoa taarifa kuwa haitokubali kuingiliwa na mataifa ya
kigeni katika masuala yake ya ndani ya nchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni