Waandaaji wa sherehe katika uwanja
wa wazi nchini Taiwani wamekamatwa na vyombo vya dola vya nchi hiyo
na kuhojiwa baada ya moto kulipuka kati kati ya mkusanyiko wa watu
waliohudhuria sherehe hiyo.
Watu zaidi ya 500 walimejeruhiwa
kufuatia tukio hilo, kufuatia poda yenye rangi kuwaka moto baada ya
kurushwa na mtammbo uliokuwa kwenye jukwaa kuelekea kwenye mkusanyiko
wa watu.
Picha zilizopigwa zinaonyesha watu
wakiwa wamechanganyikiwa na kupiga mayowe ambapo maboya ya kulalia ya
kujaza kwa upepo yalitumika kama machela za kubebea majeruhi.
Kufuatia tukio hilo watu 182 wamelazwa kwenye chumba cha wagonjwa
mahututi.
Watu waliokuwepo kwenye sherehe hiyo wakilia kwa uchungu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni