Kiongozi wa wabunge waliowengi
Bungeni nchini Kenya, Aden Duala ameibua mjadala mpya kuhusiana na
ziara ya rais Barack Obama, na kuapa kuwa serikali ya Jubilee kamwe
haitokubali shinikizo la kuridhia sera za ndoa za jinsia moja.
Duale amesema Kenya ni taifa
linalomuogopa Mungu, hivyo halitoyumbushwa na kuwa na sera ambazo
zinaenda kinyume na imani za dini, kauli ambayo ameitoa wakati rais
Obama akitarajiwa kuitembelea Kenya Julai 25 na 26.
Rais huyo wa taifa la Marekani
amepagiwa kukutana na rais Uhuru Kenyatta, pamoja na viongozi wa
vyama vya upinzani nchini Kenya, hata hivyo agenda za mikutano yao
hazijajulikana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni