Watu wanaoishi katika mji wenye
hoteli ya kitalii ya Sousse nchini Tunisia wamefanya maandamano
kupinga kitendo cha kuuwawa watu 38, wengi wao wakiwa watalii na mtu
mwenye silaha siku ya Ijumaa.
Kundi lingine la watu lilikusanyika
katika hoteli hiyo iliyoshambuliwa na mshambuliaji mwanaume mwenye
silaha, ili kupaza sauti zao za kupinga kitendo hicho.
Maandamano hayo katika mji huo
yalikuwa yamejawa na majonzi kutokana na mauaji hayo, ya watu ambayo
miongoni mwao wapo raia wa Uingereza 15.
Mtuhumiwa aliyefanya shambulizi hilo akiwa na silaha aina ya AK 47
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni