Dunia inaingia
katika kipindi cha kutoweka, utafiti uliofanywa na vyuo vya Marekani
umethibitisha ambapo imeelezwa binadamu ndio atakuwa miongoni mwa
wahanga wa mwanzo.
Ripoti ya utafiti
huo iliyoongozwa na vyuo vikuu vya Stanford, Princeton na Berkele
umesema wanyama wenye uti wa mgongo wamekuwa wakitoweka kwa kiwango
cha mara 114 kwa kasi kuliko kawaida.
Matokeo ya utafiti
huo yanaungana na ripoti iliyochapishwa na Chuo Kikuu cha Duke mwaka
jana. Mmoja wa wachapishaji wa ripoti hiyo amesema tunaingia katika
hatua ya sita ya kutoweka kwa wingi mno.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni