Idadi ya watu waliokufa katika tukio
la moto kwenye kituo cha mafuta katika Jiji la Accra nchini Ghana
imefikia watu 150.
Moto huo uliotokea jumatano umetokea
wakati watu wakikabiliana na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa
iliyonyesha kwa siku mbili, iliyowaacha watu wengi bila ya makazi,
wala umeme.
Mafuriko yamekuwa yakiathiri
jitihada za kuokoa watu, na huenda ndio yaliyochangia kutokea mlipuko
wa moto huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni