Polisi nchini India inawashikilia
wanaume watatu wanaotuhumiwa kwa kumteka mwandishi wa habari na kisha
kumchoma moto hadi kufa.
Mwandishi wa habari huyo Sandeep
Kothari alitekwa akiwa katika jimbo la nyumbani kwao la Madhya
Pradesh siku ya Ijumaa.
Vyombo vya habari vimesema Kothari
huenda amefanyiwa unyama huo kutokana na kuandika juu ya uchimbaji
madini haramu, na kufuatilia kesi inayohusiana na kosa kama hilo
iliyopo mahakamani.
Kifo cha Kothari ni tukio la hivi
karibuni linaloibua tatizo la kushambuliwa vibaya waandishi wa habari
nchini India.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni