Zaidi ya watu 120 wamekufa kutokana
na joto kali nchini Pakistani katika mkoa wa kusini wa Sindh.
Maafisa wa afya wamesema idadi kubwa
ya vifo vimetokea Jijini Karachi, ambalo limekuwa na joto linalofikia
nyuzi joto 45 kwa siku za hivi karibuni.
Mji huo wa Karachi umekuwa tatizo la
kukatika kwa umeme, lililochangiwa na ongezeko la mahitaji ya umeme
kutokana na hali ya joto kali.
Mkuu wa kitengo cha dharura katika
hospitali ya Jinnah jijini Karachi amesema wengi wa wahanga wa joto
kali ni wazee.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni