.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 11 Juni 2015

ZSSF YATANGAZA MAFAO YA UZAZI KISIWANI PEMBA

WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, wakifuatilia mada juu ya mafao ua uzazi, kwenye mkutano wa siku moja ulioandaliwa na ZSSF na kufanyika jengo la ZSSF mjini Chake Chake Pemba, (Picha na Bakar Mussa, Pemba).
KATIBU Tawala mkoa kusini Pemba, Ahmed Khalid Abdalla akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, juu ya elimu ya mafao ya uzazi, mkutano huo ulifanyika jengo la ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA uhusiano na masoko wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, Mussa Yussuf Mussa, akielezea namna mfuko huo uliovyojipanga kwa ajili ya kutoa mafao ya uzazi kwa wanachama wake, kwenye mkutano uliojumuisha pia wanachama wa mfuko, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mipango, uwezeshaji na utafiti wa Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF, Khalifa Muumini Hilali, akielezea chimbuko la mafao ya uzazi, kwenye mkutano wa kuelimishwa wanachama juu ya dhana hiyo, mkutano huo ulifanyika jengo la ZSSF mjini Chake Chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MDAU wa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF ambae hakupatikana jina lake, akiuliza suali kwenye mkutano wa kuelimishana juu ya mafao ya uzazi, mkutano huo ulifanyika jengo la ZSSF mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba). Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni