.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Julai 2015

AZAM Vs YANGA NANI MKALI?

Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC. 

Mechi hiyo ya pili inatarajiwa kuanza saa 10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kufuatia timu hizo mbili zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na upinzani mkali kuanzia katika Ligi Kuu a Vodacom Tanzania na michuano mingine.

Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema hana cha kuogopa katika mchezo huo dhidi ya Yanga, vijana wake amewandaa kupambana katika hatua hiyo ya robo fainali na ana imani wataibuka na ushindi.

Stewart ameongeza kuwa ana wigo mpana wa kikosi chake, katika hatua ya makundi wameweza kushinda michezo yao yote mitatu na kufunga mabao 8, huku ukuta wake ukiwa haujaruhusu bao hata moja kuingia wavuni kwake.

Kwa upande wa Yanga, kocha Hans Van der Pluijm amesema naaiheshimu klabu ya Azam, na katika mchezo wa kesho hana cha kupoteza, kikosi chake kimemalilika kila idara kuelekea katika hatua ya robo fainali.

Hans anajivunia kikosi chake ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kutoka mchezo wake wa awali iliyoupoteza, na kushinda michezo mitatu mfululizo iliyofuatia katika hatua ya makundi.

Mchezo wa kwanza wa robo fainali utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy ya Sudan, mechi itakayoanza saa 7:45 mchana uwnaja wa Taifa jijini Dar es aalaam.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB nchini Tanzania Ineke Bussemaker anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali kesho kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.

 
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni