Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava , akiongea jambo wakati akifungua kikao kazi baina ya REA taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo , Taasisi Binafsi , Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Edmund Mkwawa, katikati ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini (REA), Dr. Lutengano Mwakahesya na mjumbe wa Bodi ya REA, Dr. Gideon Kaunda.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijjini (REA), Dr. Lutengano Mwakahesya akiongea jambo wakati wa kikao kazi baina ya REA taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo , Taasisi Binafsi, Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao kikao kazi baina ya REA, taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo n, Taasisi Binafsi, Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, (katikati) katika picha ya pamoja na Washirika wa Maendeleo
Mwenyekiti wa Bodi ya REA Edmund Mkwawa, akiongea jambo wakati wa kikao kazi baina ya REA, taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo na Taasisi Binafsi, Wizara , Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Taasisi za Kifedha, Taasisi Binafsi na Washirika wa Maendeleo nchini, wameshauriwa kuona fursa zilizopo katika sekta ya nishati hususani umeme kushirikiana na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ili kuwezesha mapinduzi ya maendeleo na kuhakikisha kwamba vijiji vingi zaidi vinaunganishwa na nishati ya umeme.
Hayo yamebainishwa nyakati tofauti katika kikao kazi kilichoandaliwa na REA, kikijumuisha Taasisi za Kifedha, Taasisi Binafsi, Washirika wa Maendeleo Washirika katika tasnia ya nishati, wawakilishi kutoka Wizara na Taasisi za Serikali, kwa lengo la kujadili na kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikiana pamoja na kuongeza nguvu ili kuhakikisha kwamba Tanzania hususan vijiji vinaunganishwa na nishati ya umeme ikiwemo kuchochea shughuli za kiuchumi vijijini kupitia nishati hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava amesema miradi ya kuviunganisha vijiji na nishati ya umeme ni eneo linalohitaji kuendelezwa kwa ushirikiano na wadau hao ili kuongeza kasi ya uunganishaji umeme.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya REA Edmund Mkwawa, ameeleza kuwa, endapo wadau hao watashirikiana na REA, mradi huo utaleta matokeo makubwa zaidi ya yaliyopatikana sasa na hivyo kuweza kuyafikia maeneo ambayo hayajafikiwa na nishati hiyo. Aliongeza kuwa, zipo fursa nyingi ambazo taasisi hizo zinaweza kuzitumia kupitia miradi mbalimbali ambayo itaziwesha kupata faida.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini (REA), Dr. Lutengano Mwakahesya alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wote ambao wamewezesha Wakala huo kuunganisha miji na vijiji na nishati hiyo na kufikia asilimia 40 na kueleza kuwa, Wakala huo utaendelea kutafuta wafadhili ili kuweza kufanikisha malengo yake ya kuhakikisha kwamba taifa linaunganishwa na umeme.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi anayeshughulikia nishati kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB), Stella Mandago, amezitaka taasisi hizo kufanya kazi na Wakala huo kwani zipo fursa nyingi na hivyo itawezesha taasisi hizo kupanua wigo wa shughuli zao kupitia nishati ya umeme.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni