Bilionea wa Saudi Arabia Prince
Awaleed bin Talal amesema atachangia dola bilioni 32 kwa taasisi za
misaada.
Mwana huyo wa familia ya kifalme
ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa kabisa duniani, amesema
amevutiwa kufanya hivyo na taasisi ya Gates Foundation, ya Bilionea
Bill na Melinda Gates.
Prince Awaleed amesema fedha
atakazotoa zitatumiwa kuchochea ufahamu tamaduni mbalimbali,
kuwawezesha wanawake, kutoa misaada kwa waathirika wa majanga pamoja
na mambo mengine.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni