Misri imesema jeshi lake litaendelea
na kupambana katika rasi ya Sinai, baada ya mapigano na kundi la Dola
ya Kiislam (IS), yaliyopelekea vifo vya watu zaidi ya 100.
Jeshi la Misri limesema operesheni
ya kijeshi haitositishwa hadi hapo magaidi wote watakapofagiliwa
mbali katika eneo hilo.
Jeshi limesema wanajeshi 17 ni
miongoni mwa watu waliouwawa baada ya wapiganaji wa IS kufanya
mashambulizi mawili karibu na eneo la ukaguzi huko Sheikh Zuweid na
Rafah.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni