Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameapa
kushiriki binafsi kikamilifu katika kupambana na tatizo la ulevi
pamoja na uuzaji wa pombe haramu.
Rais Kenyatta amesema mapambano
dhidi ya pombe haramu yataanzia eneo la kati la Kenya kwa kuwa ndilo
lililoathirika mno kwa ulevi, na pia yatasambaa katika maeneo mengine
ya nchi.
Ameelezea kuwa uuzaji wa pombe zenye
sumu pamoja na pombe zenye madhara nchini Kenya kuwa ni biashara ya
kifo, na kusema anaanzisha kampeni ya siku nne eneo la kati la Kenya.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni