Madaktari Diaspora Washinton wakiwa katika bandari ya Zanzibar wakijiandaa kurudi nyumbani baada ya kumaliza ratiba yao Tanzania ya kutoa huduma ya Afya kwa Wananchi wa sehemu hizo mbili wakiwa Tanzania wameletwa na Jumuiya ya Watanzania Washington wakiongozana na Rais wa Jumuiya hiyo Ndg Iddi Sandaly na Mjumbe wa Kamati Bi Asha Nyanganyi. Zanzibar walikuwa wageni wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Madaktari hao wakiwa katika bandari ya Zanzibar wakijiandaa kurudi nyumbani kwa boti ya Kampuni ya Azam Marine Kilinanjaro v.
Wakiwa katika chumba cha VIP katiba bandari ya Malindi Zanzibar wakisubiri taratibu za usafiri bandari hapo ili kurejea nyumbani.
Mjumbe wa Kamati ya Jumuiya ya Watanzania Washington Asha Nyanganyi akiwa na ujumbe huo.
Wakiwa katika chumba maalum cha VIP katika bandarini malindi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanmzibar Ndg Adila Hilal Vuai Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington Ndg Iddi Sandaly na Afisi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Salum Ramia wakibadilishama mawazo katika ukumbi wa VIP bandari kupongezana kufanikisha ziara hii muhimu kwa Wananchi wa Zanzibar kupata tiba na ushgauri nasaha juu ya magonjwa ya Meno, Saratani ya Matiti na Kisukari.
Picha kwa hisani ya ZanziNews
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni