Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mh Edward Ngoyai Lowassa atangaza rasmi kuondoka Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) na kutangaza kujiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) kuanzia leo.
Ametangaza uamuzi huo mbele ya viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa ) toka vyama vya Chadema, Nccr Mageuzi, Cuf na Nld waliohudhuria mkutano huo.
Asema safari ya matumaini inaendelea na kuwataka watanzania kujitokeza kujiandikisha kwa wingi ili kutimiza azma hiyo ya safari ya matumaini kwa kuiondoa CCM madarakani.
Katika hotuba yake, Mh Lowassa alisema mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM.
Amekabidhiwa rasmi kadi ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Mh Freeman Mbowe
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni