Makaburi sita yaliyozikwa watu
wengi yamebainika kusini mwa jimbo la Guerrero nchini Mexico, wakati
wa msako wa wanafunzi 43 wa ualimu waliotekwa mwezi Septemba mwaka
jana.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imesema
mabaki ya miili 129, imebainika kutoka kwenye makaburi hayo.
Hata hivyo hakuna hata mwili mmoja
wa mabaki hayo, uliohusishwa na wanafunzi hao 43 ambao hawajulikani
iwapo wapo hai ama wamekufa tangu watekwe eneo la Iguala.
Kwa mujibu wa taarifa, kati ya miili
129 iliyokutwa kwenye makaburi hayo, 112 ni ya wanaume, 20 wanawake
na wengine waliobakia hawajatambulika jinsia zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni