Mbunge wa Kongwa
aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amempiga mgombea mwenzie kwa
nafasi ya ubunge, Dk. Joseph Chilongani kwa madai ya kumpiga picha
wakati anafanya fujo kwenye mkutano wa kampeni wa kura za maoni.
Tukio hilo
limetokea jana jioni wakati wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM
wakiwa kwenye mkutano na wanachama wa CCM kwa ajili ya kujinadi
kwenye kata ya Ugogoni iliyopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa
shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mdogo wa Dk. Chilongani, Michael
Chilongani, Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya mmoja wa wagombea
anayeitwa Simon Ngatunga kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kuahidi kuwa kama
atakuwa mbunge atahakikisha kuwa anaziba mianya yote ya ubadhirifu
kauli iliyomkera Job Ndugai.
Ilipofika zamu ya
Ndugai kujinadi kwa wanachama wa CCM alimtuhumu Ngatunga kwa kusema
uongo na kwamba hakuna ubadhirifu wa aina yoyote ndani ya Halmashauri
hiyo na aliposhuka jukwani Ndugai alianza
kumtafuta Ngatunga ili ampige kwa fimbo ambayo huwa anatembea nayo
kwenye kampeni hizo.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo
alisema kuwa hana taarifa kuhusiana na tukio hilo ambapo Job Ndugai
simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni