Bunge la Uganda limepitisha sheria
ambayo inapiga marufuku uingizaji, utengenezaji, usambazaji, umiliki
aman uuzaji wa kifaa cha kuvutia tumbaku kwa njia ya bomba maarufu
kama Shisha nchini humo.
Sheria hiyo imekuja kutokana na
wabunge kuonyeshwa kuguswa na ongezeko la athari za kiafya nchini
Uganda zitokanazo na tumbaku inayowekwa ladha na kutumika kwenye
kifaa hicho, ambayo inamadhara kuliko sigara.
Chini ya sheria hiyo iwapo utatiwa
hatiani kwa kosa la kuwa na kifaa cha kuvutia Shisha, utakwenda jela
kwa kipindi cha miezi sita, au kulipa faini ya shilingi 480,000 za
Uganda ama adhabu zote mbili kwa pamoja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni