Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Lowassa amechukua fomu hio Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wanachama wa Chadema na viongozi wa juu wa Chama hicho.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache mara baada ya
kuchukua Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA).
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza jambo baada ya kumkabidhi fomu Edward Lowassa kugombea Urais.
Mwanasheria
mkuu wa Chadema Mhe. Tundu Lissu akiongea katika hafla fupi ya
Mhe.Edward Lowassa wakati akichukua fomu katika ofisi za Chadema makao
makuu jijini Dar e salaam
Lowassa, (kulia), akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba kuwania urais kupitia CHADEMA, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.
Mwenyekiti
wa Chadema (Kushoto) Mhe. Mbowe akizungumza jambo na Mhe. Edward
Lowassa wakati wa zoezi la kuchukua fomu lililofanyika makao makuu ya
Chadema.
WAZIRI
Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, (kulia), akionyesha mkoba wenye fomu
za kuomba kuwania urais kupitia CHADEMA, baada ya kukabidhiwa na
Mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, kwenye makao makuu ya
chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2015. Mh
Lowassa, alijiunga hivi karibuni na chama hicho, baada ya kujitoa CCM.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe (Wa kwanza kushoto) akizungumza na Edward Lowassa pamoja na mke wake Regina Lowassa (wa kwanza kulia) walipowasili katika ofisi za Chadema makao makuu kwa ajili ya kuchukua fomu, (Wa pili kushoto) ni naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
Mmoja wa wana CCM ajitokeza kumuunga mkono Mh Edward Lowassa katika kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CHADEMA, Huku wanachama wa CHADEMA wakimpongeza kwa kumbeba juu juu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni