Ijumaa, 31 Julai 2015
TIMU YA TAIFA YA NGUMI YAANZA VYEMA MASHINDANO YA NGUMI AFRIKA MASHARIKI YANAYOFANYIKA MOMBASA, KENYA
Wachezaji wa timu ya Taifa ya ngumi waliokwenda Mombasa Kenya kuwakilisha Taifa katika mashindano ya kimataifa ya nchi za Afrika Mashariki wameanza vizuri kupeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano yaliyoanza leo tarehe 30/07/2015 jijini Mombasa kwa kushirikisha nchi za Tanzania, Uganda na wenyeji Kenya, Timu hiyo yenye jumla ya mabondia wanne na kocha Saidi Omari iliondoka juzi kwa udhamini wa viongozi wa juu wa shirikisho la masumbwi Tanzania.
Matokeo kwa michezo waliyocheza mabondia kutoka Tanzania yalikuwa kama ifuatavyo:-
· Katika uzito wa 49 Kgs Gerevas Logasian(TAN) alishindwa na Mwinyifiki Kombo wa (Kenya) kwa majaji 3.0,
· 52 Kgs. Said Hofu (TAN) alimshinda Sajabi Yassini (Kenya) kwa majaji 2,1
· 56 Kgs Hamadi Furahisha (TAN) alimshinda Denis Ochieng (Kenya) kwa majaji 3.0 kwa
· 60 KGS Ismail Issack (TAN) alimshinda Mava Johnboscow (Uganda) kwa TKO
Mashindano hayo yataendelea kesho tarehe 31/07/2015 kwa hatua ya nusu fainali na fainali za mashindano hayo zitafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 01.08.2015 na timu kurejea nyumbani 02.08,2015.
Lengo la mashindano ni kuziandaa timu za kutoka ukanda wa Afrika mashariki vizuri kabla ya kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa hususani Mashindano ya Afrika ( All African Games).
Shirikisho la ngumi Tanzania linawatakia mafanikio zaidi ili kutangaza vema Tanzania kupitia mchezo wa ngumi
Habari hizi zinaletwa kwenu na
Makore Mashaga
KATIBU MKUU.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni