Mmoja wa mabalozi wa kidoti aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari.
Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A hii leo wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao.
Mabalozi wa kidoti wakiwa kazini.
Baadhi ya bidhaa zinazosambazwa nakidoti jijini Arusha
Hizi ndizo ndala za kidoti Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
Wito umetolewa kwa vijana ndani ya jiji la Arusha kujitokeza katika kuchangamkia fursa za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza kuwaepushia vijana na matendo maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya jamii kukosa thamani.
Wito huo umetolewa na Joketi Mwigelwa (kidoti) wakati akichagua vijana wajasiriamali ndani ya jiji la Arusha katika ukumbi wa triple A jijini hapa ambapo anatarajia kuwapata wajasiriamali vijana ambao hatawaingiza katika fursa ya wajasiriamali kwa kupitia kampuni yake ya kidoti.
Alisema kuwa amevutiwa kuja kuwekeza ndani ya jiji la Arusha katika nyanza za ujasiriamali kwa kuwa anaelewa kuwa vijana wa jiji la Arusha hususa ni wasichana wana muitikio mkubwa katika swala zima la ujasiriamali na maendeleo binafsi.
Aidha alibainisha kuwa katika mchakato huo wanatarajia kupata wajasiriamali wapatao 13 ambapo tofauti na kujiingizia kipato cha ujasiriamali pia watakuwa mabalozi wa kutangaza bidhaa zilizo chini ya kampuni ya kidoti.
“ndugu mwandishi unavyowaona hawa wote hapa ni vijana kutoka mkoa mzima wa arusha na mikoa ya jirani tunawafanyia usaili na kupata vijana ambao wanakithi vigezo vya kuingia katika ujasiriamali ,utakao
wapelekea wao kufanya kazi na kampuni ya kidoti pamoja na kujiajiri binafsi” alisema kidoti
Pamoja na hayo alisema kuwa kampuni hiyo kwa mwaka huu imeamua makusudi kusogeza huduma za ikiwemo bidhaa zake katika mikoa ya nje ya jiji la Dar Es Salaam ili kuwapa furusa watu wa mikoani ambao walikuwa hawazipati huduma za kidoti.
Kwa upande wa mmoja wa washiriki waliojitokeza katika mchujo huo Anolia Agustino alimpomgeza kidoti kwa hatuqa aliofikia ya kuwaajiri vijana haswa wasiochana kwani ,jambo hili litawasaidia wanasichana
wengi kupata ajira pamoja na kujiajiri binafsi.
Aidha alisema kuwa mbali na kupata ajira pia kampuni hii itawasidia kujifunza ujasiriamali pamoja na kujiajiri binafsi kwani ,bidhaa za kidoti ni za bei na fuuu na unaweza kuanza kujiajiri kwa kutumia mtaji mdogo.
Kwa upande wa mshiriki mungine ambaye teari alikuwa amenufaika na kampuni ya kidoti aliyejitaja kwa jina la Anjela Mushi alisema kuwa kampuni hii imemsaidia sana kwani alikuwa anakaa nyumbani bila kazi lakini alivyoona kwenye mtandao wa kijamii aliamua kujitafuta mawasiliano na kuanza na mtaji mdogo na kwasasa ivi mtaji wake umekuwa.
“mimi nilianza kuona bidhaa za kidoti katika mitandao ya kijamii kama intagramu nikaamua kutafuta mawasilano kwakeli nilipata na nilikuwa na mtaji mdogo kwani nilianza na mtaji wa shilingi laki moja na sasa na shilingi laki nne na biashara yangu nilianza mwezi wa tano na sasa ni mwezi wa saba kwa hadi sasa nina mienzi mitatu nashukuru mungu
mtaji wangu umekuwa”alisema Anjela.
Alimalizia kw akumpongeza kidoti na kumsihi aendelee kuwasaidia wasichana kwani hivi sasa kumekuwa na changamoto ya ajira kwani ajira imekuwa ni ngumu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni