Polisi wa Ufaransa wamelazimika
kutumia mabomu ya machozi pamoja na ya kupulizia kwa kundi la
wahamiaji ambao wamekuwa wakikatiza kwa nguvu kuingia katika kito cha
reli cha kuelekea Uingereza.
Polisi hao wamekuwa wakitumia
virungu vyao kujaribu kuwazuia wahamiaji hao wazivuke uzio wa usalama
kuelekea kwenye usafiri wa treni ya Ulaya.
Mashahidi wamesema wahamiaji hao
wamekuwa wakikimbia katika eneo hilo mithili ya wacheza soka, huku
polisi wa kutuliza ghasia wakijaribu kuwadhibiti kutoingia kwenye
eneo la njia ya reli.
Wahamiaji wakipiga mahesabu ya kuwapita polisi
Chini ya ulinzi...polisi akiwa anamdhibiti chini mhamiaji
Wahamiaji wakisaidiana kupenya kwenye fensi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni