Kiongozi wa upinzani nchini Burundi
Agathon Rwasa amechaguliwa kuwa naibu spika wa bunge la nchi hiyo,
licha kukosolewa mno kwa uchaguzi wa wabunge na wa rais nchini humo.
Kumekuwepo na mgogoro wa kisiasa
tangu rais Pierre Nkurunziza atangaze kuwania tena urais kwa muhula
wa tatu.
Rwasa ambaye alijitoa mwezi uliopita
katika uchaguzi wa rais na kuuelezea ushindi wa Nkurunziza kama
mzaha, amekubali nafasi hiyo na kusema ataitumia kurejesha amani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni