.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 6 Julai 2015

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AFUTARISHA MKOA WA KUSINI UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilali wakati wa futari aliyoitayarisha kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika jana katika viwanja vya Jengo la Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiitikia Dua baada ya Swala ya Magharibi iliyoswaliwa katika viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati wakati wa futari aliyoitayarisha kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilali (kushoto) pamoja na Viongozi wengine katika futari aliyoitayarisha kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika katika viwanja vya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati jana
Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Jengo la Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati jana
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akiwa Waziri wa Kilimo na Maliasili Sira Ubwa Mamboya (kulia) na Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohammed katika futari iliyotayarishwa kwa Wanannchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana katika Ukumbi wa Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati
Akinamama wa Vijiji tofauti vya Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika Ukumbi wa Ofisi ya Jengo la Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija alipokuwa akitoa shukurani kwa niaba ya Wananchi na Viongozi wa Mkoa wake jana baada ya futari waliyaalikwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Wananchi wa mbali mbali wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya futari ya pamoja aliyoitayarisha kwa Wananchi hao iliyofanyika jana katika viwanja vya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati,[Picha na Ikulu.]

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni