.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 4 Julai 2015

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AFUTURU NA WANANCHI WA KIJIJI CHA MKANYAGENI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akishiriki katika swala ya magharibi iliyoswalishwa na Sheikh Chumu Salim kabla ya futari aliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba jana katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.

WANANCHI wa Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba wamepongeza juhudi kubwa zilizochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein za kuhakikisha amani, utulivu na mshikamano miongoni mwa wananchi vinaimarika kwa lengo la kuleta maendeleo.

Hafla hiyo ya futari ilifanyika katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni, na kuhudhuriwa na wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani pamoja na viongozi mbali mbali wa Mkoa huo pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali.

Aidha, Mama Mwanamwema Shein naye aliungana pamoja na akina mama wenzake wa kijiji hicho cha Mkanyageni katika futari hiyo ya pamoja.

Wananchi hao waliyasema hayo wakati wakitoa neno la shukurani katika futari maalum walioandaliwa na Alhaj Dk. Shein hapo kijijini kwao Mkanyageni ikiwa ni utamaduni aliouweka wa kufutari nao pamoja kila ufikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akitoa neno hilo la shukurani kwa niaba ya wananchi wa Mkanyageni, Maalim Abdalla Yussuf alisema kuwa katika uongozi wa Alhaj Dk. Shein wananchi wameshuhudia mshikamano mkubwa sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu ambavyo ndio dira ya maendeleo.

Maalim Abdalla alisema kuwa mbali ya shukurani kwa futari hiyo aliyowaandalia pia, wananchi wa Mkanyageni wanatoa shukurani za pekee kwa Alhaj Dk. Shein kwa kuifanyia mema Zanzibar.

Mara baada ya futari hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdalla alitoa shukurani kwa wananchi wote waliohudhuria katika hafla hiyo.

Alhaj Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza ushirikiano na mshikamano uliopo miongoni mwa wananchi wa Zanzibar sambamba na kuendelea kuishi kwa amani na utulivu.

                                                                                      Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni