Rais Yoweri Museveni wa Uganda
amechangia kiasi cha shilingi milioni 400 katika ujenzi wa jengo la
ofisi zitakazotumiwa na wasanii wa nchini Uganda.
Museveni ni mpenzi wa muziki na
aliachia wimbo wake wa 'Mpenkoni' miaka mitano iliyopita na hivi
karibuni ameachia wimbo wa 'Yengoma' kwenye You Tube ambao umepata
watu 6,100 na kupakuliwa mara 7,500 hadi kufikia mwishoni mwa wiki
iliyoisha.
Rais Museveni ametangaza mchango wake huo wa fedha baada ya wasanii wa muziki na sanaa kumuomba kuwatafutia eneo la ardhi kwa ajili ya kujenga jengo la makao makuu ya wasanii nchini Uganda.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni