Mahakama nchini Libya imemuhukumu
mtoto wa Kanali Muammar Gaddafi, Saif al-Islam pamoja na watu wengine
wanane hukumu ya kifo kwa kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa
vuguvugu la mapinduzi ya umma mwaka 2011.
Katika kesi hiyo pia wamo makumi ya
watuhumiwa ambao walikuwa washirika wa karibu wa serikali ya marehemu
Kanali Gaddafi, ambao wanatuhumiwa kwa kutumia nguvu kudhibiti
waandamanaji wakati wa vuguvugu la nguvu ya umma.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa mtoto huyo wa Kanali Gaddaf, Saif al-Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia video.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa mtoto huyo wa Kanali Gaddaf, Saif al-Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia video.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni