Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni 237.
Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Wawekezaji wote wananufaika kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni