Mamia ya wahamiaji wameangusha uzio
wa fensi kuelekea katika njia ya reli usiku wa jana wakati wakikatiza
kujaribu kuwahi kupanda treni kuelekwa Kent katika safari
iliyobatizwa jina la kuingia Uingereza ama kifo.
Wabunge waandamizi wa Uingereza
wamesema jeshi la Uingereza linapaswa kupelekwa kuwadhibiti wahamiaji
hao kwa kuwa inaonekana mamlaka za Ufaransa zimezidiwa na kushindwa
kuwazuia.
Hali hiyo imechangia maafisa polisi
wa kutuliza ghasia wa Ufaransa 120 kupelekwa katika eneo hilo, ili
kusaidiana na askari kanzu 250 walipo katika eneo hilo, hata hivyo
idadi hiyo inasemekana haitoshi.
Wahamiaji wanawake wakikatiza juu ya uzio
Mhamiaji akipenya kwenye tundu katika uzio huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni