Muwindaji anayetuhumiwa kumsaidia
mtalii Mmarekani kumuua simba maarufu nchini Zimbabwe ameachiwa hutu
kwa dhamana.
Muwindaji huyo Theo Bronkhorst
amekiri kosa la kushindwa kuzuia uwindaji haramu, na kuachiwa kwa
dhamana ya kiasi cha dola 1,000.
Bronkhorst pamoja na mmiliki wa
kapuni yake Honest Ndlovu wataitwa tena mahakamani Agosti 5.
Mmarekani Walter Palmer, ambaye ni
daktari wa maneo aliyemuua simba huyo aitwae Cecil kwa kumpiga risasi
ameondoka nchini Zimbabwe lakini naye atakabiliwa na mashtaka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni