Watu 4 wamefariki dunia papo hapo na wengine 30 wamejeruhiwa baada ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kugonga basi la abiria lililofahamika kwa jina na Badikadi mkoani Morogoro.
Taarifa za awali toka kwa mashuhuda na majeruhi wa ajali hiyo wamesema kuwa, ajali hiyo imetokea eneo la njia panda kibaoni katika kijiji cha Kibaoni, kata ya Mpakani.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, dereva wa basi hilo lililokuwa linatoka Kilosa kuelekea Morogoro mjini alitaka kuvuka njia ya treni bila kuwa muangalifu ndipo basi hilo lilipogongwa na treni hiyo ya mizigo.
Majeruhi wote hivi sasa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Kilosa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni