Muigizaji filamu Lupita Nyong'o
ametajwa kuwa balozi wa kimataifa wa tembo, baada ya kuonekana kwa
mara ya kwanza jana nchini Kenya tangu ashinde tuzo ya Oscar.
Ziara yake hiyo ni ya kwanza kwa
muigizaji huyo katika nchi ya wazazi wake, baada ya kushinda tuzo
hiyo ya juu kutokana na uhusika wake kwenye filamu ya 12 Years a
Slave.
Akiongea mbele ya vyombo vya habari
Lupita amesema anajivunia kuwa Mkenya na kuwa balozi wa Kimataifa wa
kupambana na mauaji ya tembo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni