Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis
Tsipras, amesema wananchi wa taifa hilo wamefanya uamuzi wa busara
kwa kupiga kura ya kupinga masharti ya kimatiafa ya kuisaidia
kuikomboa kiuchumi.
Matokeo ya mwisho ya kura ya maoni
yanaonyesha asilimia 61.3 ya wananchi wa Ugiriki wamekataa masharti
ya kimataifa na asilimia 38.7 wameridhia masharti.
Maelfu ya wananchi wa Ugiriki
wamekuwa wakisherehekea uamuzi huo mitaani wakipeperusha bendera,
wakipaza sauti zao na kufyatua fashifashi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni