Waziri Mahmoud akipokea funguo za gari gari kwa niaba ya Wizara ya Afya kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika hilo Dkt. Khalfan Abdallah Mohamed na kuliahidi Shirika la SCI kuzitunza ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
Gari hizo mbili zitagawiwa ambapo Unguja itabakia moja na Pemba kupelekwa moja ili kusaidia mapambano ya Maradhi yasiyopewa umuhimu.

Shirika
la Shistosomiasis Control Initiative (SCI) la Uingereza limetoa Msaada
wa Magari mawili aina ya Toyota Double Cabin kwa Wizara ya Afya Zanzibar
kupitia kitengo chake cha Maradhi yasiyopewa umuhimu (NTD).
Akikabidhi msaada huo leo Mwakilishi wa Shirika hilo Dkt. Khalfan Abdallah Mohamed amesema lengo la Msaada huo ni kuiwezesha Zanzibar kupiga hatua katika mapambano yake na Maradhi hayo ambayo yanawaandama watu wengi.
Maradhi hayo ni pamoja na Matende, Minyoo,Kichocho ambayo ni vigumu kupata Misaada ya matibabu kutoka kwa Wafadhili wa jumuiya za kimataifa.
“Ni rahisi sana kuomba Msaada wa Maradhi kama UKIMWI kwa vile yanapewa kipaumbela na Wafadhili lakini maradhi mengine kama Minyoo au Matende ni vigumu sana kumshawishi mfadhili akasaidia” alisema Mwakilishi huyo wa SCI.
Imetolewa na Maelezo Zanzibar

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni